Walimu bora na wenye uzoefu
Shule ina walimu wa kutosha wenye uzoefu na ubobevu wa hali ya juu wa kufundisha
Shule ya msingi ya St.Getrude inamilikiwa na shirika la Masista wa Benediktini wa Imiliwaha , shule ilianzishwa mwaka 2009 ikiwa na usajili wa namba Rv 02/3/001 na baadae ikabadilishwa namba ya usajili EM.14700 .Shule ya St.Getrude ni ya bweni na kutwa huchukua wanafunzi kuanzia chekecheka wenye umri wa miaka minne . Shule hii ipo barabara kuu kutoka Songea Mjini kwa km 88 kuelekea Makambako. Shule ya msingi St.Getrude ipo katika kijiji cha Ndelenyuma km . 03 kando ya barabara kuu katika kata ya Mkongotema Halmashari ya Madaba mkoa wa Ruvuma.
Shule ina walimu wa kutosha wenye uzoefu na ubobevu wa hali ya juu wa kufundisha
Shule ina viwanja vya michezo na vifaa vingine kwa ajili ya michezo kwa wanafunzi wetu
Tuna huduma zote za muhimu kama maji, umeme, chakula bora na malazi
Tuna mahitaji mbalimbali ya shule kama vitabu na vitu vingine vya kujifunzia